Jamaa
mmoja amenaswa nchini Saudi Arabia, wakati akijaribu kuingiza nchini
humo zaidi ya makopo 48,000 ya bia aina ya Heineken, yaliyozibwa na
kufanana na soda aina ya Pepsi (PICHANI), katika taifa hilo la kiislam
lililoko Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu.
Pamoja na kuwa adhabu za makosa kama hayo hutofautiana ni kinyume cha sheria kukutwa na pombe katika Ufalme wa Saudi Arabia.
Kwa
mujibu wa Mtandao wa LBC America, maafisa ushuru katika mpaka wa Al
Batha walikamata shehena hiyo ilipokuwa ikijaribu kupenya na kuingia
nchini humo.
“Gari
lililobeba iliyodhaniwa kuwa na shehena ya vinywaji vya Pepsi
lilisimamishwa na baada ya utaratibu wa kawaida wa kukagua bidhaa hiyo
ilibainika kuwa ni pombe iliyovalishwa stika ya ilizibwa na karatasi ya
Pepsi” alikaririwa akisema Meneja Mkuu wa mpaka wa Al Batha, Abdulrahman
al-Mahna
Afisa
huyo pia alikaririwa akisema kuwa pamoja na jitihada, ubunifu na ujanja
wa kuingiza bidhaa nyingi zilizopigwa marufuku, askari doria wake “siku
zote wako tayari kukamata bidhaa hizo”
Hata hivyo haijajulikana bado mtuhumiwa huyo atachukuliwa hatua gani kwa kitendo hicho.
Post a Comment