Mahakama
ya ardhi na nyumba mkoa wa Arusha imeamuru mzee wa miaka themanini Juma
Isangu aliyeondoshwa kwa nguvu katika nyumba yake arudi kwenye nyumba
yake na arudishiwe vyombo vyake wakati ikisubiriwa kuanza kusikilizwa
kwa shitaka la msingi huku Bi Jane Fosbroke na wakala wa mahaka majembe
Auction Malt wakitakiwa kulipa ghalama za usumbufu kwa mzee Juma Isangu.
Akitoa
amri hiyo mwenyekiti wa mahakama ya ardhi na nyumba mkoa wa Arusha
Cyriacus Kamugisha amesema kutokana naombi liliowakilishwa na upande wa
mashitaka mahakama imeyapitia kujirishisha na kufanya uamuzi huo kwa
kuzingatia misingi ya kisheria.
Wakizungumza
baada ya kutoka kwa amri hiyo mawakili wa wanao mtetea mzee Juma Isango
Willifredy Milambo na Loam Ojale wamesema wamezidhika na uamuzi wa
mahakama kwakuwa awali mteja wao hakutendewa haki kwa kuondoshwa kwa
nguvu katika nyumba yake huku akiwa na nyalaka zilizo halali huku Bi
Janeth akieleza kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama.
Kwa
upande wao watetezi wa haki za wazee wamesema ikiwa mahakama
zitafanyakazi kwa uadilifu na kuharakisha maauzi kama ilivyo fanya kwa
mzee huyo zitarudisha imani kwa wananchi huku wakiipongeza mahakama hiyo
kutenda haki kwa mzee Isangu na majira wa mzee huyo ambayo wamehifadhi
familia yake baada ya kunyanganywa nyumba wametoa shukurani kwa uamuzi
uliyo tolewa na mahakama ikiwa ni pamoja na kumpatia wakala wa mahakama
atakaye rudisha vyombo vya mzee Isangu
Post a Comment