Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Mama Cookie’mpenzi wake, Moses Iyobo ‘Mozes’.
BAADA
ya kuanika picha za gari lake jipya aina ya Audi A4 kwenye akaunti yake
ya mtandao wa kijamii wa Instagram akimshukuru mpenzi wake, Moses Iyobo
‘Mozes’ kwa kumzawadia ‘mkoko’ huo, staa wa sinema za Kibongo, Aunt
Ezekiel Grayson ‘Mama Cookie’ anadaiwa kuhongwa gari hilo na kigogo.
Mara tu baada ya ‘kuposti’ picha za gari hilo, baadhi ya mashabiki wa Aunt ambao ni watu wake wa karibu…
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Mama Cookie’mpenzi wake, Moses Iyobo ‘Mozes’.
MWANDISHI WETU
BAADA
ya kuanika picha za gari lake jipya aina ya Audi A4 kwenye akaunti yake
ya mtandao wa kijamii wa Instagram akimshukuru mpenzi wake, Moses Iyobo
‘Mozes’ kwa kumzawadia ‘mkoko’ huo, staa wa sinema za Kibongo, Aunt
Ezekiel Grayson ‘Mama Cookie’ anadaiwa kuhongwa gari hilo na kigogo.
Mara
tu baada ya ‘kuposti’ picha za gari hilo, baadhi ya mashabiki wa Aunt
ambao ni watu wake wa karibu waligawanyika, wapo waliodai gari hilo
lilitokana na kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wengine walidai
amehongwa bila kumtaja mtu aliyemuhonga.
“Jamani
Aunt si useme tu kuwa gari umehongwa? Usimsingizie Moze Iyobo na kama
si hivyo basi ni fedha ulizopata kwenye kampeni si bure,” alisema mmoja
wa mashabiki wake hao.
Alipobanwa
na mwandishi wetu, Aunt alifunguka kwamba, hana la zaidi kwani
ameshaweka wazi gari hilo amelitoa wapi na asiyeamini abaki hivyohivyo.
“Nimenunuliwa
na baba Cookie, hayo mambo yenu ya kampeni mimi siyajui wala sijahongwa
kwani hakuna mwenye ubavu wa kunihonga kwa sasa,” alisema Aunt.
Post a Comment