Watu sita wamefariki dunia baada ya gari ndogo waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la abiria mali ya kampuni ya Princess Muro, lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Tunduma, katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, barabara kuu ya Morogoro-Iringa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa
ajali hiyo katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, ikihusisha gari
ndogo la abiria aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 359 BBA
iliyokuwa imebeba abiria sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume wanne
ambayo ilipasuka tairi ya Mbele ya kuyumba ovyo barabarani na kugongana
na basi hilo la Princess Muro lenye namba T 160 BBC na kusababisha vifo
kwa abiria wote wa Noah.
Amesema
basi hilo la abiria aina ya Zangton lililoharibika zaidi mbele huku
Noah ikiharibika kabisa, likuwa likiendeshwa na Silos Wilfred (55) mkazi
wa Mbeya ambaye anahojiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, na kwamba
basi alilokuwa akiendesha lilikuwa na abiria 59 ambao hawakupata madhara
makubwa, isipokuwa michubuko kidogo kwa baadhi yao na walitafutiwa
usafiri kuendelea na safari.
Katika
upekuzi wa miili ya abiria waliokuwa kwenye Noah inayodaiwa kuhusika na
ubebaji wa magazeti, viligundulika vitambulisho vimne vya Ali Nduti
Mohamed (27), mkazi wa Mbeya,Sani Elion Mkwabe (24) mkazi wa Kunduchi,
Patrick Mkelegene (43) mkazi wa Buguruni Malapa na Selemani Omary (30)
ambaye makazi yake hĂ yajaweza kujulikana Mara moja.
Miili ya watu hao waliopoteza maisha imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Post a Comment