MWIGIZAJI ambaye
inaaminika kwa muda mrefu hajawahi kuvaa nguo yenye mpasuo kiasi cha
mapaja yake kuonekana, Halima Yahya ‘Davina’, amefunguka kuwa kwa mara
ya kwanza Jumapili iliyopita alilazimika kuvaa nguo iliyoonesha sehemu
ya paja lake kutokana na mazingira ya pati ya mwigizaji mwenzake, Wema
Sepetu ‘Madam’.
Akielezea
vazi hilo alilolitinga katika sherehe ya kuzaliwa ya Madam, Davina
alisema kwa mazingira ya pati hiyo yenye hadhi ya aina yake, alilazimika
kuvaa nguo hiyo ili kuendana na mazingira lakini si kwamba amebadilika
tabia yake.
“Jamani
pale nilivaa tu kulingana na mazingira na hata hivyo haijaanika mapaja
kihivyo, si kwamba ndiyo nimebadilika kitabia, kamwe siwezi kubadilika,”
alisema Davina.
Post a Comment