Maandalizi ya fainali ya shindano la Miss Universe Tanzania 2015 bado
yanaendelea Mwanamitindo wa Kimataifa Miriam Odemba atakuwa jaji maalum
katika kinyang’anyiro hiki cha kumpata mrembo wa Miss Universe Tanzania
2015.
Zoezi la usaili limeshakamilika na hatimaye kupata warembo watakaojiunga na kambi ya Miss Universe kesho siku ya jumatano kabla ya fainali tarehe 20 mwezi huu.
Warembo waliobahatika kuingia kambini ni 14 tu, majina na mikoa waliyotoka kwenye mabano Mariam Isack (Dar es salaam), Lilian Luth(Dar es salaam), Stacey Sulul(Dar es salaam),Willice Donard(Dar es salaam), Lorraine Marriot(Dar es salaam), Dalena David(Dar es salaam), Mercy Zephania(Dar es salaam), Dinnah Kaijage(Dar es salaam), Melody Typhone(Dar es salaam), Joselyn Mirashi(Arusha), Nancy Matta(Mbeya), Christina Shimba(Iringa), Belinda (Mwanza).
Mwaka huu Miss Universe imefanya usaili katika mikoa sita tofauti ikiwamo Tanga, Iringa, Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es salaam.
Post a Comment