Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JOSE MARA,KALALA JR KUREJESHA MAPACHA WATATU


Tatu


babuseya4Msanii wa muziki wa Dansi Bongo, Joseph Michael ‘Jose Mara’.
Wasanii wa muziki wa Dansi Bongo, Joseph Michael ‘Jose Mara’, na Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, Jumamosi hii (leo) wanatarajia kuirejesha  bendi yao ya Mapacha Wanne, ambayo ilikuwa ikiundwa na mastaa wenzao wawili Khaleed Chuma ‘Chokoraa’ na Junior Kalala ‘Kalala Junior.’


TatuMapacha Watatu (Jose Mara, Khalid Chokoraa na Kalala Junior).
Wasanii hao usiku wa leo watafanya makamuzi ya pamoja ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya mwendelezo wa kundi hilo ambalo lilisamb- aratika baada ya Chaz Baba kuzuiwa na bendi yake ya zamani  ya African  Stars ‘Twanga Pepeta’, huku Kalala Junior naye akijiengua kwenye bendi hiyo na kuwaacha Jose Mara na Chokoraa.
Akizungumza na gazeti hili Jose Mara alisema leo watawakumbusha mashabiki zao namna walivyokuwa  wakifanya wakati wapo kwenye kundi moja,  mbali na hivyo pia itakuwa ni mwanzo wa kujenga umoja wa Mapacha Wanne, kwani wanatarajia kupiga shoo zaidi ya moja nje ya Jiji la Dar.
“Kweli leo Mapacha Wanne itarudi kwani tutafanya makamuzi ya nguvu hivyo  nawaomba watu waje kutushuhudia kwani  tutakuwa tukitoa burudani na kujenga umoja wa Mapacha Wanne, tutasindikizwa na  Twanga Pepeta,” alisema Jose Mara.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top