Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC AMOS MAKALA KWAKE NI KAZI TU!!

Mkuu mpya wa Mkoa waKilimanjaro Mh. Amosa Makalla akiongea na menejimenti. 

Mkuu wa Mkoa Makalla akijikinga na mvua kubwa.

Mkuu wa Mkoa Makalla akiwa kwenye njia ya kuanzia kupanga mlima sehemu Marangu.

Mkuu wa Mkoa Makalla Akikagua kitabu utaratibu wa kusajili watalii.


Mkuu wa Mkoa Mh. Makalla, akiongea na watalii toka Ireland.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla ametembelea Hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA)na kufanya kikao na menejimenti ya  kinapa, kukagua njia wanazopita watalii, utaratibu wa kuwapokea na kuwapandisha watalii mlima Kilimanjaro
Ameipongeza Kunapa kwa kuwa miongoni mwa hifadhi 5 zinazojiendesha vizuri na kuchangia mapato ya serikali, kuchangia ajira zaidi ya 100,000 kwa mwaka na usimamamizi madhubuti wa sheria za uhifadhi wa mazingira na kuanza kurejesha hali ya theluji ya mlima kilimanjaro iliyoanza kupungua kwa muda mrefu
Katika ziara hiyo ameiagiza menejimenti kufanya yafuatayo
1. Kusimamia kwa nguvu zote eneo la hifadhi lisiingiliwe na shughuli za kilimo, ujangili man uharibifu wa vyanzo vya maji
2. Kufanya mikutano na vijiji vyote 80 vinavyozunguka hifadhi kwa lengo la kuelimisha umma faida na hasara zitakazopatikana baada kuharibu mazingira
3.Kuwafungia na kuwanyanganya leseni makampuni yanayopandisha watalii yanayotuhumiwa kwa udanganyifu , utapeli unaopelekea watalii kukosa huduma na kutapeliwa
Aidha amewataka wananchi wa mkoa kilimanjaro kuendelea kupanda miti na kulinda mlima kilimanjaro na vyanzo vya maji
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top