Upande
wa Jamhuri katika kesi inayomkabili mwanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia
Tanzania (DIT), Benedict Ngonyani, anayetuhumiwa kusambaza taarifa
katika mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ), Jenerali, Davis Mwamunyange, amelishwa sumu,
umewasilisha mahakamani kusudio la kukata rufaa kupinga mshtakiwa huyo
kupewa dhamana.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage,
ilitengua hati ya kuzuia dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo iliyowasilishwa
na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP).
Kabla ya uamuzi huo, hakimu alisikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili na alikubaliana na maombi ya utetezi ya kumpa dhamana kwa kuwa sababu za DPP kuzuia dhamana hiyo hazikuwa na msingi wa kisheria.

Wakili
wa Serikali Mkuu, Theophil Mutakyawa aliwasilisha kusudio hilo jana saa
7:00 mchana, kwamba upande wa Jamhuri haujaridhika na uamuzi wa
mahakama kutengua hati ya DPP.
Pia, kupitia kusudio hilo, upande wa Jamhuri unapinga Mahakama ya Kisutu kutengua hati hiyo na kwamba haina mamlaka ya kuoindoa kwa kuwa huondolewa na DPP ama kesi inapomalizika na kutolewa hukumu.
Pia, kupitia kusudio hilo, upande wa Jamhuri unapinga Mahakama ya Kisutu kutengua hati hiyo na kwamba haina mamlaka ya kuoindoa kwa kuwa huondolewa na DPP ama kesi inapomalizika na kutolewa hukumu.
Awali
hakimu alisema mshtakiwa ni mwanafunzi na shtaka analoshtakiwa nalo
linadhaminika kwa hiyo haoni haja ya kukosa masomo yake ya darasani
Katika
kesi hiyo, inadaiwa Septemba 25, mwaka huu, jijini Dar es Salaam,
mshtakiwa alisambaza taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya
Mtandao kifungu cha 16 ya mwaka 2015 kuwa Jenerali Mwamunyange
amenyweshwa sumu.
Post a Comment