Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi (
picha ya Maktaba) ametoa wito kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Ofisi
zake kutekeleza kwa vitendo dhana ya uwazi na uwajibikani kama
yanavyozishikiza Nchi Wanachama, kwa kile alichosema, utekelezaji wa
dhana hiyo haupashwi kuwa jukumu la Serikali peke yake. Ametoa wito huo
wakati wa majadiliano ya Ripoti ya Baraza la Haki za Binadamu
iliyowasilishwa siku ya jumatatu mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa.
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, imetoa wito kwa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa, ikiwamo Baraza la Haki za Binadamu kuitekeleza kwa vitendo
dhana ya uwazi na uwajibikaji.
Tanzania
imesisitiza pia kwamba, haitoshi kwa Mashirika hayo kuzitaka
nchi wanachama kwa maana ya serikali kuwajibika na kuwa wazi katika
utekelezaji wa majukumu yake ili hali yenyewe yanafanya kinyume.
Wito
huo umetolewa siku ya Jumatatu na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,
wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lilipopokea na kujadili Ripoti
ya Mwaka ya Baraza la Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.
Balozi
Manongi ambaye alikuwa miongoni mwa Mabalozi kati ya wengi
waliochangia Ripoti hiyo iliyowasilishwa na Rais wa Baraza la Haki
za Binadamu Bw.Joachim Rucker .Amesema, Tanzania inatoa wito huo
kutoka kile kinachoonekana dhahiri kwamba ama Mashirika hayo
yamekuwa yakionyesha kuegemea upande mmoja dhidi ya mwingine au
kupendelea nchi moja dhidi ya nyingine kitendo ambacho kinakwenda
kinyume na kile wanachokihubiri.
Akatoa
mfano kwa kusema, wakati Rais wa Baraza la Haki za Binadamu
akisisitiza katika ripoti yake umuhimu wa uwajibikaji, Ofisi ya Haki za
Binadamu katika mwezi Octoba ikishirikiana na UNICEF na Canada,
ilidhamini onyesho la Filamu kuhusu kijana kutoka Geita mwenye
alibinisim, pasipo Taasisi hiyo kuujulisha Uwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania ili hali wakijua Tanzania ilikuwa mlengwa wa filamu hiyo.
“ Akiwasilisha Taarifa yake mbele ya Baraza hili mwanzoni mwa mkutao
huu, Raisi wa Baraza la Haki za Binadamu amesisitiza umuhimu wa
uwazi na uwajibikaji. Cha kusikitisha tukio la konyeshwa kwa filamu
ambayo maudhui yake yalihusu Tanzania na sisi kama Tanzania
hatukujulishwa, hakika inakwenda kinyume kabisha na dhana ambayo Rais
wa Baraza la Haki za Binadamu amekizungumza hapa” akasema Balozi
Manongi.
Na
kuongeza “ ndiyo maana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa wito kwa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa au Ofisi zake kuonyesha kwa vitendo
dhana ya uwazi, uwajibikaji na kutoegemea upande wowote”.
Akabainisha
kuwa, Mashirika ya Umoja wa Mataifa hayapashwi kujionyesha kuwa
yanaegemea upande wowote au hata kupendelea baadhi ya nchi wanachama
dhidi nchi nyingine na hasa pale ambapo Mashirika hayo binafsi
hayajapitia na kujiridhisha juu ya kile ambacho wanataka kukiunga mkono
au kutaka kujihusisha nacho.
Akaeleza
Zaidi mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba,
Tanzania haikupinga na wala haipingi filamu kuhusu kijana wa Geita,
filamu iliyolenga katika kuonyesha changamoto zinazowakabili watu
wenye ualibino nchini Tanzania.
“
Tulichopinga na tunachopina ni maelezo yaliyoandikwa na muandaaji wa
filamu hiyo, maelezo ambayo yalikuwa na upotoshaji mkubwa. Kwa mfano,
baadhi ya maelezo ya filamu hiyo yanasema, hakuna utashi wa
kisiasa kutoka Serikali ya Tanzania katika kukabili uovu wanaotendewa
watu wenye ualibino.
Kwamba,
msukumo kutoa mataifa ya nje ni wa lazima ili kutokomeza uovu huo,
kwamba ujinga ni laana kubwa inayowakabili waaafrika na jawabu
pekee ni kuwaelimisha, kwamba filamu hiyo ilikuwa ni kuwashawishi watu
wa nje ili kuleta mabadiliko ya kweli. Na vilevile filamu hiyo ilikuwa
ni kusherehekea roho ya utu na kazi nzuri inayofanywa na watu wa
Canada katika kuwasaidia watu wenye ualibino” akasisitiza Balozi
Manongi.
Akasema
Baloz, Ni kwa kuzingatia upotoshaji huo na mwingine ulioelezwa na
muandaaji wa filamu hiyo, haishangazi kuona kwamba Uwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania haukualikwa kufadhili onyesho la filamu hiyo
iliyoonyeshwa Umoja wa Mataifa.
“
Rais wa Baraza la Haki za Binadamu pia amezungumzia wajibu wa Asasi
za Kijamii katika uhamasishaji wa haki za Binadamu. Tunakubaliana na
pendekezo wake. Wakati tunauga mkono mchango wa Asasi za kijamii, ni
lazima basi Asasi hizo nazo zikaonyesha uwajibikaji na uwazi pamoja na
kujipambanua katika utekelezaji wa majukumu yao. Uwajibikaji hauwezi
kuwa ni jukumu la serikali peke yake” akasisitiza Balozi Manongi.
Akizungumzia
Zaidi kuhusu changamoto zinazowakabili watu wenye ualibino, Mwakilishi
huyo wa Tanzania, amesema, Tanzania kwa kutambua changamoto kubwa za
kijamii na kiuchumi pamoja na upatikanaji wa haki za msingi kwa watu
wenye ualibino ndiyo maana kwa kushirikiana na Malawi imeamua
kuwasilisha mbele ya Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Azimio kuhusu watu wenye ualibino.
Amesema
dhumuni kuu la Azimio hilo na ambalo linatarajiwa kupitishwa wiki hii
ni kupanua wigo na ushiriki mpana wa wadau mbalimbali ukiwamo
Umoja wa Mataifa katika kuzikabili changamaoto zinazowakabili watu
wenye ualibino.
Na
kwa sababu hiyo, Balozi Manongi ameziomba nchi wanachama wa Umoja
wa Mataifa, kuunga mkono azimio hilo pamoja na jitihada
zinazofanywa na Serikali ya Tanzania pamoja na Chama cha Watu wenye
Ualibino Tanzania (TAS) katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto
zinazowakabili watu wenye ualibino vikiwamo vitendo vya kikali
wanavyofanyiwa na watu wasio na mapenzi mema.
Post a Comment