Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maji,
Athumani Sharif akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu mikakati ya Serikali kutatua tatizo la upatikanaji wa
maji jijini Dar es Salaam mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto
ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
(Picha na Fatma Salum.)
Na. Georgina Misama - Maelezo
SERIKALI
inatarajia kuzalisha maji lita milioni 270 kwa siku baada ya
kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa Chanzo cha Maji cha Ruvu Chini na
upanuzi wa mtambo wa kusafishia maji.
Mradi
huo unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kimarekani
la Millenium Challenge Co-operation umegharimu kiasi cha shilingi
bilioni 66.24 na unatarajiwa kukamilika wakati wowote baada ya
kukamilika kwa kazi ya kulaza bomba linalosafirisha maji toka Ruvu chini
kuja Jijini Dar es Salaam.
Akiongea
na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maji, Bw. Shariff Athumani
amesema kwamba mradi wa upanuzi wa mtambo wa ujenzi wa bomba la Ruvu
Chini utapunguza kero ya maji kwa wakazi wote wanaotumia maji kutoka
Ruvu Chini.
Akiyataja
maeneo yatakayofaidika na kukamilika kwa mradi huo ni pamoja na
Bagamoyo na vitongoji vyake, Bunju, Mabwepande, Boko, Tegeta Kunduchi na
Mbezi Beach. Maeneo mengine ni pamoja na Mbezi Juu, Salasala, Kawe,
Makongo, Chuo Kikuu, Mikocheni, Msasani, Masaki, Mwananyamala,
Kinondoni, Magomeni, Sinza, Manzese, Ubungo, Mabibo, Kigogo, Buguruni,
Ilala, Kurasini, Bandarini na maeneo yote ya katikati ya jiji la Dar es
Salaam.
Post a Comment