Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani
akizugumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya viti maalumu
vya Udiwani ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na Tume hiyo ni viti
1393, kutoka katika Vyama vya CCM,CHADEMA,NSSR-MAGEUZI pamoja na
CUF.Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam ,Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Huduma za Sheria wa NEC Emmanuel Kawishe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi( NEC) imesema hadi sasa viti maalumu vya Udiwani
ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na Tume hiyo ni viti 1393, kutoka
katika Vyama vya CCM, CHADEMA, NSSR- MAGEUZI pamoja na CUF.
Hayo
yamesemwa leo Jijijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka
NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akitoa taarifa kwa Umma kuhusu uteuzi
wa madiwani wanawake wa Viti Maalumu.
Aidha
Bw.Ramadhani amesema kuwa idadi ya Viti maalumu Vya Udiwani ni 1,408
nakwamba kutokana na majimbo nane na kata thelathini na Nne ambapo
Uchaguzi haujakamilika kwa Sababu mbalimbali, hatua hiyo itasababisha
kubakia viti 15 ambavyo vitagawanywa mara baada ya Uchaguzi kukamilika
ili kufikia idadi ya viti 1,408 kutoka viti 1393 vinavyo tambulika kwa
sasa.
Aidha
amefafanua kuwa kutokana na Viti hivyo Maalumu Vya Udiwani
Vilivyoteuliwa na NEC, Chama Cha Mapinduzi CCM kimepata viti
1,022,Chama Cha Demokrasia na Mawendeleo CHADEMA 280,Chama Cha Wananchi
CUF-79, ACT WAZALENDO viti 6 pamoja na NSSR MAGEUZI viti 6.
Amesema
kuwa tume imeamua kutoa taarifa ya uteuzi wa viti maalumu Vya Udiwani
Nchi nzima ya Madiwani waliyoteuliwa na Tume kutokana na Kanuni za
Kudumu za Mikutano ya Halmashauri, Mabaraza ya Madiwani yanatakiwa
kuitishwa siku thelathini tangu tarehe ya Uchaguzi ifanyike.
Katika
hatua Nyingine Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi NEC amesema kuwa mwisho wa
Uchaguzi katika Majimbo na Kata ambazo hazikufanya Uchaguzi ni Desemba
20 mwaka huu, ambapo katika jimbo la Uranga Mashariki pamoja na Lushoto
uchaguzi utafanyika Novemba 22 mwaka huu,nakuwaomba Wananchi kujitokeza
kwa wingi kupiga kura ili kuchagua kiongozi wanaomtaka.
Post a Comment