Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Trafiki 78 wafukuzwa kazi Mwanza

 
 
ASKARI 78 wa usalama barabarani Mkoa wa Mwanza, wameondolewa katika nafasi zao na kupangiwa kazi nyingine katika vitengo mbalimbali kutokana na utovu wa nidhamu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo, akizungumza na waandishi wa habari leo, amesema mabadiliko hayo yamefanywa baada ya askari hao kujulikana hawafuati maadili na sheria za jeshi hilo.
Mkumbo amesema kuwa askari waliondolewa nafasi hizo na kupangiwa vitendo vingine ni 78, huku akisema kwamba wilaya ambayo haijafanyiwa mabadiliko ni Ukerewe kati ya saba za mkoa huo.
“Tumefanya mabadiliko haya ni ya kawaida tu, tumefanya hivyo ili kuleta utendaji wenye tija, baada ya kubaini kuna mapungufu kwa askari hao na tusingeendelea kuwa nao kwa kuwa ni watovu wa nidhamu.
“Wilaya ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Nyamagana askari 19, Ilemela 23, Sengerema 15, Magu 15, Misungwi na Kwimba mmoja (1), wilaya ambayo haijaguswa ni Ukerewe,” amesema Mkumbo.
Hata hivyo Mkumbo amesema kuwa kabla ya kufanyika kwa mabadiliko hayo, walianza kutoa mafunzo kwa askari waliochukua nafasi hizo, kabla hawajaingia barabarani.
Mkumbo amesema kuwa kabla ya mabadiliko hayo mkoa wa Mwanza ulikuwa na trafiki 249, na kwamba waliyoondolewa katika nafasi hizo ni askari wa kawaida na vyeo mbalimbali.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top