Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima John Aloyce kwa tuhuma za matumizi mabaya ya shilingi Milioni 450 zilizotumika kujenga ukumbi wa mikutano badala ya nyumba za watumishi.
Uamuzi wa Mkuu huyo wa Mkoa kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Itilima,unatokana na kiasi cha shilingi Milioni 146 kuelekezwa katika ujenzi ukumbi wa mikutano badala ya lengo la Serikali la kujenga nyumba za watumishi ili kuondoa changamoto ya watumishi kuishi nje ya Wilaya hiyo, hatua ambayo inailazimu Halmashauri hiyo kutumia zaidi ya shilingi Milioni tatu kila Mwezi kama gharama za kukodi gari kila siku kwa ajili ya kuwapeleka kazini watumishi na kuwarejesha makwao.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka pia ametangaza kufuta posho kwa Wakuu wa Idara na Vitengo ambao watakuwa wakihudhuria vikao vya kamati na mabaraza ya Madiwani katika Halmashauri zote za Mkoani huo.
Kabla ya kusimamishwa kazi,Mkurugenzi huyo Bw.John Aloyce akapewa nafasi ya kujitetea ambapo amekiri kupokea fedha hizo na kuzielekeza katika ujenzi wa ukumbi ili kupata mahali pa kukusanyia matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 Mwaka jana na shughuli mbalimbali za Halmashauri hiyo.
Nafasi ya Mkurugenzi huyo imekaimiwa na Afisa Afya na Usafi wa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Kelisa Wambura wakati uchunguzi ukiendelea kufanyika dhidi ya Mkurugenzi huyo.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
Alfajiri3 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
Serikali yatoa kauli kuhusu Dbi ya Kariakoo9 months ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-



Post a Comment