Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FATUMA KARUME ALIPUKA TENA ..... AFUNGUKA MAZITO

  Mtoto wa Kigogo wa CCM ambaye ni Mwanasheria Fatuma Karume AMELIPUKA, unaweza kusema. Akihojiwa na DW amesema sasa Zanzibar wanaishi kama wanyama maana hawafuati katiba. "Kama wameamua kuondoa utaratibu tuliyojiwekea sasa tuna tofauti gani na wanyama?"

Alipoulizwa kama vitisho vya CCM havimtishi na kama baba yake hamdhibiti, amesema. "Mimi siyo mbwa wala paka, nina haki yangu ya asili ya kujieleza na kutoa maoni" Amesema babake hawezi kuondoa uhuru wake kisa CCM.
"Wanataka baba anidhibiti? (kicheko) "nina miaka 46, tena baba ananihimiza kufanya nachoamini ni haki"

Alipoulizwa maoni yake kuhusu MCC amesema anasikia watu wanasema wazanzibar wako tayari kufa njaa lakini serikali iachwe huru. "Hivi tunahitaji serikali huru au watu huru? hapa tuna wakoloni wengine" Ameuliza "yaani watu wa Zanzibar wafe njaa kisa Shein awe rais?" haiwezekani!...
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top