Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa VPL
Pluijm amesema wamefanya maandalizi ya kila aina katika kujiandaa kuwavaa Al Ahly ikiwa ni pamoja na kuwasoma katika mechi zao mbili walizocheza dhidi ya Recreativo Libolo ya Angola ambapo sasa wachezaji wake wanatakiwa kwenda kuyafanya kazi uwanjani aliyowaelekeza.
Amesema Al Ahly ni timu nzuri yenye safu ya ushambuliaji yenye kasi ambapo mabeki wake wanatakiwa kuhakikisha hawaruhusu makosa kufanyika huku pia wakitakiwa kutumia vyema nafasi zao uwanjani.
“Hii ni mechi ngumu tunacheza dhidi ya timu tunahitaji kuwaheshimu lakini sio kuwaogopa, tumefanya maandalizi lakini hii ni hatua moja mechi ni kitu tofauti na mazoezi, nafurahi kuona morali iko juu kwa vijana wangu sasa ni wakati wa kutafsiri tuliyoelekezana mazoezini kuja uwanjani,” amesema Pluijm.
“Kikosi kipo imara ni watu wawili tutakaowakosa ukiacha Haruna (Niyonzima) ambao ni Mbuyu (Twite) mwenye maralia na Matheo (Simon) aliyepata maumivu ya mguu wake wengine wote wako salama.”
Kikosi kitakachoanza kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly mechi itakayochezwa kwenye uwanja wa taifa kimepangwa kama ifuatavyo;
Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Haji,Vicent Bossou, Kelvin Yondani, Thabani Kamusoko, Salum Telela, Simon Msuva, Deus Kaseke, Donald Ngoma na Amissi Tambwe.
Post a Comment