Kwa mujibu wa chanzo makini, Dick na mwanamke wake wa sasa wamekuwa wakimtumia meseji za matusi Shamsa kitendo ambacho mwigizaji huyo alikuwa akikivumilia lakini katikati ya wiki hii, uvumilivu ukamshinda, akaamua kwenda kumshtaki.
“Yaani hakuna kitu ambacho Shamsa alikuwa hakipendi kama kutumiwa meseji na mzazi mwenzake huyo na mwanamke wake zikimtusi kwa maana alivumilia mpaka akachoka, akaona bora aende polisi kumshtaki,” kilisema chanzo.
Shamsa Ford enzi akiwa na mzazi mwenziye Dick Matoke.
“Polisi wanaendelea kumtafuta na mpenzi wa Dick aliyekuwa akishirikiana naye kumtukana Shamsa ili naye waweze kumhoji kisha hatua nyingine za kisheria zichukue mkondo wake,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Shamsa kuhusiana na sakata hilo, alikiri kutokea lakini akaomba muda ili alizungumze vizuri kwa kile alichosema yuko bize na shughuli zake za filamu.
“Mh! Umeipata hiyo na wewe? Nani aliyekuambia? Any way ni kweli imetokea lakini nitakuelezea vizuri nikitulia, niko bize kidogo na kazi,” alisema Shamsa.
Post a Comment