Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa,
Akizungumza kutoka eneo la tukio Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa, amesema mawasialiano hayo yamekatika katika eneo la Chalinze Nyama ambapo abiria na magari hayo yamekwama kuanzia Alfajiri ya leo.
Bi. Zamaradi amesema mpaka sasa Askari wa Usalama barabarani wameshafika eneo la tukio kwa ajili ya kuangalia ni jinsi gani wanaweza kutatua tatizo hilo kwa haraka ili abiria waendelee na safari.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema maji hayo yameharibu kabisa miundo mbinu katika baadhi ya maeneo na kusababisha adha kubwa ya usafiri katika Mikoa hiyo ambapo mpaka wanausalama wanaendelea na jitihada za kutatua adha hiyo iliyowakumba wananchi wengi zaidi.



Post a Comment