Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS MAGUFULI AFUTA SHEREHE ZA MUUNGANO .... AELEKEZA PESA ZA SHEREHE ZIKAPANUE BARABARA YA MWANZA


Rais John Magufuli ameahirisha shamrashamra za kikukuu ya kumbukumbu ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambazo hufanyika kila mwaka, Aprili 26.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Rais Magufuli amewataka wananchi kusherehekea siku hiyo kwa kupumzika majumbani kwao na katika shughuli zao binafsi.

Aidha, fedha zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya kugharamia vyakula, vinywaji, gwaride na mengineyo ameagiza zielekezwe katika upanuzi wa barabara ya Mwanza ‘Mwanza – Airport’, katika eneo linaloanzia Ghana Quarter hadi katika uwanja wa ndege jijini humo, kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari.

Hii  ni Taarifa Rasmi toka Ikulu 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top