Ama kweli penzi ni kikohozi, kulificha huwezi. Baada ya usiri mzito kutawala, hatimaye imebainika kuwa The Big Boss wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ndiye ‘aliyeinjinia’ penzi jipya mjini la muigizaji Jacqueline Wolper na kijana anayekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva, Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’.
RISASI LILIANZA KUTONYWA
Awali, gazeti hili lilitonywa kuhusu penzi hilo jipya na chanzo chake makini na kueleza namna ambavyo Diamond alivyokuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha Hamonize ambaye ni memba wa WCB ‘anamng’oa’ Wolper.
“Diamond ndiye aliyesimamia mchakato mzima. Katumia kila mbinu kuhakikisha Wolper anaingia kwenye himaya ya mdogo wake. Nafikiri pia atakuwa ameangalia na suala zima la kibiashara, muziki sasa hivi unataka msanii azungumzwe,” kilisema chanzo hicho.
DOGO NDIYE ALIANZA KUSUMBUA
“Hamonize ndiye aliyeanza kuvutiwa na Wolper. Akamwelezea Diamond hisia zake, kama unavyojua tena Diamond si mtu wa kuremba, fasta tu akaweka mambo sawa. Kila kitu kikaenda kwenye mstari,” kilisema chanzo chetu.
MKONGO HANA CHAKE
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kutokana na Diamond kumwaga ‘sumu’ za kutosha na Wolper kuingia penzini ‘mzimamzima’ ndani ya muda mfupi, Mkongo aliyekuwa anammiliki mrembo huyo hana tena chake kwa sasa.
“Aaah! Mkongo hana chake tena kwa sasa. Wolper hasikii wala haoni. Amechanganyikiwa na penzi la Hamonize kiasi ambacho hataki kusikia habari ya mwanaume mwingine yeyote,” kilisema chanzo hicho.
MAMBO HADHARANI MITANDAONI
Mara baada ya chanzo hicho kumwaga ubuyu huo, wakati Risasi Mchanganyiko likiendelea kufanya uchunguzi wake, ghafla likakumbana na video ya wawili hao kupitia mtandao wa kijamii wa ‘Snap Chat’ ambayo ilimuonesha Wolper akiwa ‘hajiwezi’ kwenye gari akiimbiwa wimbo wa Number One wa Diamond na Hamonize aliyekuwa akiendesha gari hiyo.
Chanzo:Global Publishers
Loading...
Post a Comment