Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HALI BADO TETE SAKATA LA MAUAJI DADA YAKE BILIONEA MSUYA

Ikiwa bado kuna sintofahamu ya chanzo cha mauaji ya dada yake bilionea Erasto Msuya, Anneth, Polisi wamesema hawajabaini sababu za awali za kifo hicho na wanaendelea na msako wa waliohusika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alisema hadi jana wauaji walikuwa hawajakamatwa, licha ya juhudi za upelelezi zinazoendelea.

Tukio la Anneth Msuya aliyeuawa Alhamisi usiku kwa kuchinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam, limekuwa ni mwendelezo wa matukio mengine ya uhalifu kwa familia yao yaliyowahi kutokea baada ya kifo cha kaka yake, Msuya.

Miongoni mwa wanaotafutwa na Polisi ni mfanyakazi wa ndani aliyeondoka nyumbani kwa Anneth mchana kabla ya kutokea mauaji hayo, kwa madai kuwa hawezi kuendelea na kazi na kuacha ufunguo kwa jirani.

Bilionea Msuya aliuawa Agosti 2012 kwa kupigwa risasi, tukio lililofanyika mkoani Kilimanjaro.

Ikiwa ni miaka minne tangu kifo hicho, kingine kinatokea kwenye familia hiyo.

Dada wa Anneth, Ester, anayeishi Mbezi Makonde jijini Dar es Salaam, alisema juzi kuwa mazishi ya mdogo wake yatafanyika mkoani Kilimanjaro Mei 30.

Bado watu wengi wanajiuliza kuhusu mfululizo wa matukio katika familia ya Msuya, huku wakishangaa sababu za binti huyo kuuawa kama kaka yake.

“Ni kweli kifo hupangwa na Mungu, lakini siyo kwa kifo hiki. Kwa nini wanauawa?” alihoji Juma Majuto, mmoja wa waombolezaji wa msiba huo uliopo Mbezi Makonde.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top