Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAZISHI YA MCHEKESHAJI KINYAMBE YALIVYOKUWA

MAMIA ya wakazi ya jiji la Mbeya wamemzika aliyekuwa msanii wa vichekesho James Petro Nsemwa (30) maarufu kama Kinyambe ambaye alifariki dunia jumatano ya wiki hii mkoani Mbeya, katika makaburi ya Hayombe Uyole Igawilo mkoani Mbeya.

Msururu wa wakazi wa jiji la Mbeya pamoja na magari ulitembea kutoka nyumbani kwa wazazi eneo la makondeko mtaa wa mtakuja kata ya Igawilo kuelekea makaburi ya bonde la uyole kwa umbali kilometa tatu na nusu.
Pia baadhi ya wasanii kutoka Dar es Salaam wakiongozwa na Kitale waliudhuria mazishi ya msanii mwenzao ingawa hapakuwepo na uwakilishi wa viongozi ngazi ya mkoa uliyofika mazishini.
Msiba huo uliosimamisha shughuli mbalimbali kwa muda ili kupisha msururu wa watu na magari ambao ulikuwa ukielekea makaburini yaliyopo eneo la Nsalaga.
Baba wa marehemu, mzee Lugendelo Nsemwa, amesema kuwa akiwa nyumbani kwake Uyole, kuwa mwanaye ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa uchekeshaji, alianza kuumwa tangu Juni mwaka jana, ambapo moyo, tumbo na miguu ilikuwa imejaa maji pamoja na pafu la kushoto.
Alisema tatizo hilo lilipelekea mapafu yake kushindwa kufanya kazi sawasawa.

“Kwa kipindi kirefu alikuwa amelazwa katika hospitali mbalimbali kama vile Uyole, Ifisi, Rufaa na hospitali ya mkoa wa mbeya, hali yake ilibadilika, alizidiwa na kupoteza fahamu, na bahati mbaya Jumatano saa 3 usiku akafariki dunia,” alisema mzazi huyo

Komediani huyo aliyetamba kwa kubadilisha sura na sauti yake katika filamu za uchekeshaji nchini, James Petro Nsemwa a.k.a Kinyembealizaliwa tarehe 19.09.1985 katika kijiji cha Mahanji- Matamba.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top