Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHADEMA WASEMA WATAZUIA MKUTANO MKUU WA CCM WA KUMKABIDHI MAGUFULI UENYEKITI ... WANAJIPANGA KWA HILO


 
Chama cha Demokrasa na Maendeleo Chadema kimesema hakitarusu Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi unaotarajia kufanyika tarehe 23 Julai mwaka huu kwa ajili ya kumkabidhi uongozi Mwenyekiti wa chama hicho Dkt John Pombe Magufuli kutokana na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kutawanya mikutano ya chama hicho na kuzuia mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu. 

Katibu Mkuu wa Baraza la vijana Chadema taifa  Julius Mwita ameyasema hayo baada ya Jeshi la Polisi kuzuia mahafali ya kuwatunuku vyeti wanachama wa vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro. 

Amesema kitendo kinachofanywa na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kuzuia mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ni kukandamiza Demokrasia hapa nchini na kuwataka vijana kutokata tamaa. 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Taifa (Zanzibar) Salum Mwalimu amesema wanasikitishwa na kitendo kinachofanywa na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kutawanya mikutano ya chama hicho hapa nchini. 

Akielezea mazingira ya kuzingirwa na Jeshi la Polisi Mwenyekiti wa Bazara la vijana Chadema mkoa wa kilimanjaro Dikson Kibona amesema walishangaa kuwaona wakizingirwa huku wakipewa amri ya kutawanyika la sivyo watatawanyishwa kama hawatatii amri.
Chanzo-Itv
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top