Loading...
BREAKING NEWS .... Mwimbaji maarufu wa Taarabu, Bi Shakila amefariki Dunia
TANZIA:
Nimepata habari muda huu Muimbaji Maarufu wa Taarab Bi Shakila Said amefariki muda si mrefu.
Nimezungumza na mwanae muda huu na amethibitisha hilo.
Shakila Saidi enzi ya uhai wake akipeana mkono na aliyekuwa Rais wa JMT, Mh. Kikwete
Amefariki leo saa tatu usiku (19 Agosti) hospitali ya Temeke. Mwili umepelekwa hospitali ya Jeshi Lugalo.
Marehemu alitoka safari juzi, na leo ameanguka huko nyumbani kwake, aliwahishwa hospitali ambapo umauti umemkuta.
Marehemu Shakila ameacha familia ya watoto 13.
Taarifa nyingine zaidi baadae zitapatikana.
Inna Lillah Wa'inna Illaihi Raji'un.
C&p
Post a Comment