Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCM YAMLILIA MZEE ABOUD JUMBE

SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea jana tarehe 14thAgosti 2016 nyumbani kwake Mji Mwema, Kigamboni  jijini Dar es salaam.

Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Chama cha Mapinduzi mara baada ya kuunganisha Chama cha ASP na TANU.

Mzee Jumbe alikuwa ni Kiongozi mchapakazi, Muasisi na Mwanamapinduzi aliyeshiriki katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ametoa mchango mkubwa katika kuunganisha vyama vya TANU na ASP. Ameweka rekodi nzuri ya kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyetumikia nafasi hiyo kwa muda mrefu (1972 – 1984) na kutembelea Vijiji na Wilaya nyingi za Tanzania Bara na Zanzibar na kusikiliza kero na changamoto za wananchi.

Aidha, Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Ali Mohamed Shein, familia ya Mzee Aboud Jumbe pamoja na Wazanzibari wote kufuatia kifo cha Kiongozi wetu. Tunaungana nao katika msiba huu ambao pia ni msiba wetu.


WanaCCM nchi nzima tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.  Amina
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top