Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MGEJA AMVAA RAIS MAGUFULI


ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amesema hatua ya Rais John Magufuli kuzuia kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini, imelenga kuminya demokrasia na serikali kutaka kutokosolewa.

Mgeja, ambaye kwa sasa ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa hatua hiyo haikubaliki katika nchi ya kidemokrasia duniani kwa kuwa uhai wa vyama vya siasa upo katika mikutano.

Pia amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kushughulikia migogoro ya vyama badala ya kusubiri hadi nchi ikielekea katika mgogoro mkubwa.

Alisema kauli ya Rais Magufuli kwamba shughuli za kisiasa hadi mwaka 2020, inakiuka katiba kwa kuwa mikutano na shughuli za vyama vya siasa vipo kikatiba.

Alieleza kuwa kinachotokea sasa kwa viongozi wa upinzani ni kupigania demokrasia hali ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi.

“Serikali inakosolewa kupitia mikutano ya vyama vya siasa na serikali isitupangie cha kuzungumza. Kutokana na kauli ya rais tunaonya likitokea lolote katika mikutano ambayo itafanyika nchi nzima, kupitia operesheni ya Umoja wa Kuondoa Udikteta Tanzania (Ukuta), Rais atawajibika iwapo nguvu ya jeshi polisi itatumika,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top