Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Chadema wawapata wagombea Umeya

Dar es Salaam.  Siku saba baada ya kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni, Chadema Mkoa wa Dar es Salaam imefanya uchaguzi wa kura za maoni, kujiandaa na uchaguzi wa mameya wa Ubungo na Kinondoni.

Akizungumza baada ya kuvunjwa kwa baraza hilo, Mkurugenzi wa Kinondoni, Aron Kagurumjuli amesema uchaguzi wa kuwapata mameya na manaibu wao unatakiwa kufanyika ndani ya siku 14.

Katika kura za maoni jana, madiwani wa chama hicho wa maeneo hayo waliwapitisha Mustafa Muro kugombea Kinondoni na Boniface Jacob kuwa ni Ubungo.

Kabla ya uchaguzi wa meya, majina hayo yatapelekwa Kamati Kuu ya chama hicho kujadiliwa na kupigiwa kura sanjali na walioshika nafasi ya pili na ya tatu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top