Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Prof. Tibaijuka azidi kung'ara kimataifa

Kwa mara nyingine tena, mwanamama profesa Anna Tibaijuka, ameendelea kung'ara kimataifa baada ya kushinda tuzo ya 'His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award f or Sustainable Development'.

Tuzo hii imetolewa na Waziri mkuu wa Bahrain Mtukufu Khalifa bin Salman Al Khalifa jana tarehe 24-9-2016

Sherehe za utoaji wa tuzo hizo umefanyika katika viwanja vya makao makuu ya umoja wa mataifa New York Marekani, na kuudhuliwa na viongozi mbalimbali duniani wakiwemo mabalozi wa nchi mbali mbali, mawaziri kutoka nchi mbali mbali na viongozi wengine waandamizi.

Tanaznia iliwakilishwa na waziri wa mambo ya nje Balozi Maige pamoja na mbunge viti maalumu mama Anna Lupembe.

 Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya umoja wa mataifa, raisi wa mkutano mkuu wa umoja wa mataifa Peter Thomson amempongeza Prof. Tibaijuka kwa ushindi huo wa tuzo na kusema mwana mama huyo amekua chachu ya maendeleo edelevu kote duniani, hasa ktk kuboresha makazi ya watu kwa kipindi chote alicho tumika kama katibu mkuu mwandamizi umoja wa mataifa, mkurugenzi wa makazi duniani lakini pia waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Tanzania.

Kwa niaba ya waziri mkuu wa Bahrain, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Bahrain naye amemtaja mama Tibaijuka kama kiongozi wa mfano na wa kuigwa duniani kote kwa juhudi zake kubwa za ku support maendeleo endelevu.

Miongoni pia mwa watu mashuhuri walio hudhuria hafla hiyo ni pamoja na binti wa mfalme wa Saudi Arabia.

Sherehe hizo zimefanyika jana tarehe 24-9-2016 hapa New York UN-HQ


Angalia Video ya Sherehe hiyo..
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top