Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwenyekiti UVCCM Arusha afikishwa Mahakamani

Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya. 

Arusha. Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya leo amepandishwa kizimbani kujibu tuhuma mbili za kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa na kugushi kitambulisho cha usalama wa taifa.

Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa CCM katika Kata ya Sambasha wilayani Arumeru mkoani Arusha alikamatwa na polisi Septemba 16 na alikaa rumande kwa mahojiano hadi leo alipofikishwa mahakamani.

 Mwendesha mashitaka wa serikali, Lilian Mmasi alieleza mahakama kuwa, Sabaya alitenda kosa la kwanza Agosti 13 mwaka huu, katika nyumba ya kulala wageni ya Skyway jijini hapa.

Alisema alijifanya ni mtumishi wa  Usalama wa Taifa wa kujipatia huduma mbalimbali kwa njia ya udanganyifu.

Alisema katika kosa la pili, katika muda usiojulikana, Sabaya anatuhumiwa kugushi kitambulisho cha Usalama wa Taifa namba MT.86117 wakati akijua ni kosa la jinai kufanya hivyo.

Baada ya maelezo hayo, Sabaya alikana makosa hayo na wakili wake, Yoyo Asubuhi alimuomba hakimu mkazi  Gwantwa Mwankuga ampatie dhamana mteja wake.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top