Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC Gambo acharuka, ayageukia madeni ya Waalimu

Habari picha na Woinde Shizza,Arusha 
 MKUU wa mkoa Arusha Mhe Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai walimu ya milioni 154 ndani ya wiki mbili ambayo wamekuwa wakidai serikali kuu kwa muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi. 
Mhe. Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi. 
Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na kwamba hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu ndio inayopaswa izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufudisha na kufuatilia kila siku madeni hayo. 
 “Mkurugenzi nakupa muda wa wiki mbili deni hili la milioni 154 kwa ajili ya walimu hakikisha zinalipwa haraka iwezekanavyo wakishalipwa ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa kwani haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.

 Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa fedha hizo ambazo ni madeni hayo zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba atahakikisha kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani za halamshauri hiyo ili zikija zirejeshwe. 
Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka kwenye fedha alizoziokoa ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa madiwani ambapo kiasi cha milioni 130 zilizokuwa zinatumika kuwalipia madiwani mafuta ,simu pamoja na nauli zitaelekezwa kulipa walimu hao madai yao ili waweze kujikimu na hali wanayokabiliana nayo. 
 ‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya mafuta ni milioni 40.8,fedha za simu za madiwani milioni 61.2,nauli iliyookolewa milioni 28 ambapo jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume hivyo fedha hizi zinaelekezwa kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ikiwa ni madeni wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lkni tumeona tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha watoto wetu vizuri”alisema Kihamia . 
Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha hizo kwa walimu hao wakati wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili waendelee kujikimu kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea hivyo zitaongeza ufanisi kwa walimu katika kufundisha wanafunzi na akili zao na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili wapate elimu bora.
 Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao walisema kuwa wanakabiliwa na tatizo la kutopandishwa madaraja kwa waliokaa kazini muda mrefu huku wengine walioingia kazini muda mfupi wakiwa wanapandishwa madaraja bila kujua vigezo hivvyo kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.
 MKUU wa mkoa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiongea na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha, waratibu elimu, wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata
 Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiongea na walimu walioudhuria mkutano huo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Download Our App

1 comments:

NAMSHAURI AENDE NA WILAYANI MAANA YEYE NI MKUU WA MKOA!!!ZA WILAYANI ZINASHIDA NYINGI SANA!!!!

Reply

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top