Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wabunge wa Simba, Yanga kukipiga kuchangia wahanga tetemeko la ardhi

  Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika mchezo wao kati ya wabunge wa Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Septemba 25 katika Uwanja wa Taifa ikiwa na lengo lenye kuchangia wa wahanga wa tetemeko la Ardhi wa wamkoani Kagera, Kulia ni nahodha wa timu ya Bunge, Sixtus Mapunda na kushoto ni Mkurugenzi wa benchi la ufundi Professa Maji marefu.
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azan 'Zungu' akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuelekea Mchezo  utakaochezwa Septemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie jijini Dar es Salaam leo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanatarajiwa kucheza mechi ikiwa na lengo la kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoa wa Kagera.

Mwenyekiti wa klabu ya Michezo ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, William Ngeleja amesema kuwa mchezo huo utakaochezwa Septemba 25 katika Uwanja wa Taifa utajumuisha wabunge wanaochezea Simba na Yanga.

Ngeleja amesema kuwa, wabunge hao watacheza mchezo huo kwa pamoja ila mwaka huu kumekuwa na sura mpya nyingi sana ambazo mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa lakini lengo kuu ikiwa ni kuchangia wahanga wa Kagera.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azan 'Zungu' amesema kuwa taifa limepata janga la taifa Kwahiyo anawaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuwachangia watanzania wenzetu ambao kwa kipindi hiki wanaishi katika mazingira mabaya.

Viingilio vya mchezo huo utakuwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko kijani na bluu, 10000 na 15000  kwa  viti vya machungwa, VIP A 200,000, VIP B 100,000 na VIP C ni 50,000 huku kutakuwa na viti 50 vilivyotengwa ambapo kwa yoyote atakayekaa hapo atalipia 1,000,000.

Katika siku hiyo pia Kutakuwa na mechi ya mpira wa pete kati ya TBC na wabunnge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawake huku Wasanii wa  bongo fleva na Bongo Movie
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top