Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali yaigomea EPA

Serikali imesema kuwa haitasaini mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara na Jumuiya ya Ulaya (EPA) kwa jinsi mkataba wake ulivyo na walakini.
Serikali imesema kuwa haitasaini mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara na Jumuiya ya Ulaya (EPA) kwa jinsi mkataba wake ulivyo na walakini.

Akizungumza Alhamisi hii wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa Iringa mjini kupitia CHADEMA, Peter Msigwa, lililohoji, kwanini serikali inasuasua kusaini mkataba wa EPA pamoja na jumuiya za Ulaya, Naibu waziri wa mambo ya nje, Dkt Susan Kolimba, alisema, “sisi tunachokipigania kama wizara, kama serikali ni kwa manufaa ya nchi hii,na kwa manufaa ya wananchi.”

“Tunaposema tunasita tumesema kwamba hatusaini kwasababu mkataba ule kwa namna fulani jinsi ulivyokaa utaaffect maslahi ya watanzania na hasa katika suala zima la kuhakikisha viwanda vinaweza kuendelea na wewe unajua hilo, kwahiyo hatusaini kwasababu hiyo,” aliongeza.

Hiyo si mara ya kwanza kwa serikali kuwa na mashaka na mkataba huo wa ushirikiano wa kiuchumi. Mwaka jana, Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, alielezea kusikitishwa na jinsi Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika Mashariki, zilivyosaini mkataba huo.

Mkapa aliutaja mkataba huo kuwa ni aina nyingine ya ukoloni kama ilivyokuwa kwa mkataba wa Berlin wa mwaka 1880, ambapo nchi za Ulaya zililigawa bara la Afrika kwa ajili ya manufaa yao kiuchumi.

Alisema kupitia mkataba huo, ni vigumu kwa kampuni za kiafrika kushinda zabuni katika nchi za Ulaya lakini ni rahisi kwa kampuni za Ulaya kushinda zabuni katika nchi za Afrika kutokana na kukomaa kiteknolojia, na hata zinaposhindanishwa kampuni za Afrika na Ulaya ni rahisi kwa kampuni za Ulaya kushinda, jambo litakalochangia kuua kampuni za kiafrika.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top