Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Diwani achomwa mkuki

Kiteto. Diwani wa Kata ya Kaloleni eilayani Kiteto mkoani Manyara, Christopher Parmet amenusurika kufa baada ya kuchomwa mkuki na wafugaji wa eneo hilo wakati akifukuza mifugo iliyovamia shamba lake.

Diwani huyo ambaye ni katibu mwenezi wa CCM wilayani Kiteto na katibu wa mbunge wa jimbo hilo, Emmanuel Papian na hivi sasa amelazwa kwenye hospitali ya wilaya hiyo akipatiwa matibabu.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Papian alisema afya ya Parmet inaendelea vizuri baada ya kuongezewa damu kwani alivuja damu nyingi baada ya kuchomwa mkuki kiganjani.

Papian alisema diwani huyo alijeruhiwa jana jioni alipofika shambani kwake kwa ajili ya kuwalipa vibarua wake watatu ambao pia walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.

Baada ya tukio hilo diwani huyo alipiga simu kwa mkuu wa wilaya na kwa mbunge wa jimbo kwa ajili ya kutoa taarifa ndipo mkuu wa polisi wa wilaya akatuma gari lililowachukua na kuwafikisha hospitalini.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Francis Massawe alisema yupo nje ya nchi hivyo asingeweza kuzungumza tukio hilo.

Mganga mkuu wa wilaya hiyo Dk Lupembe alithibitisha majeruhi hao kulazwa kwenye hospitali ya wilaya hiyo na kuwa wanaendelea kupata matibabu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top