Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Spika Ndugai afumua kamati ya Bunge na kuisuka upya

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefanya mabadiliko makubwa kwenye Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, akiwabadilisha wabunge ishirini na wanne waliokuwa wanaunda kamati hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge, Ndugai ameteua wajumbe wapya kumi na sita wa kamati hiyo ambao pia watakuwa wajumbe wa kamati nyingine.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Spika ametumia Mamlaka aliyonayo kikatiba kuunda Kamati za Bunge kadri anavyoona inafaa, na kwamba mabadiliko haya yamelenga katika kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kibunge.

“Kanuni ya 116 (3) –(5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016 inampa Spika mamlaka ya kuteua wajumbe ili wawe wajumbe katika kamati mbalimbali za Bunge ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kuongeza, kubadilisha au hata kupunguza idadi ya wabunge katika kamati za kudumu za Bunge,” imeeleza taarifa hiyo.

Mabadiliko hayo yameanza mara moja kuanzia mwezi huu wa Oktoba na kwamba wajumbe wote wameshatumiwa barua tayari kwa maandalizi ya kukutana na kuwachagua viongozi wa kamati hiyo.

Hii ni orodha ya waliokuwa wajumbe wa kamati hiyo na kamati walizohamishiwa kufuatia mabadiliko hayo:
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top