Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

John Mnyika hachomoki ... Barua aliyosaini kuomba mkopo hii hapa ...

Na. Mwandishi wetu,
wakati Mbunge wa Kibamba na naibu katibu mkuu wa Chadema John John Mnyika akikana kuutambua mkopo wa milioni 300 uliokopwa na kampuni inayohusishwa kumilikiwa naye ya TESTA LIMITED huku yeye akiwa kama mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi mwenye mamlaka yote ya kiutendaji katika kampuni hiyo.

hali sasa imebadilika baada ya siri zaidi kuhusiana na ushiriki wa mbunge huyo machachari kukopa kiasi hicho cha pesa kuanza kuwekwa hadharani.

vielelezo vya kikampuni, kibenki na kimalipo ya mkopo huo na mingine kadhaa inayoihusu kampuni hiyo, vinaonyesha ushiriki wa moja kwa moja wa mbunge huyo kijana.

katika mkopo unaohusisha udhamini wa nyumba ya Erasto Tumbo ambaye wakati anaidhamini kampuni hiyo ya mnyika, alikuwa Afisa wa Uenezi makao makuu ya chadema huku Mnyika yeye akiwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi yaani bosi wake, tumbo yeye nyumba yake ilithaminishwa kwa shilingi milioni 160 na shilingi 140 zilizosalia zilisaminishwa na nyumba ya Mzee Charles Tumaini Chanika ambaye pia ni Meja Mstaafu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania.

Taatifa zinasema kuwa Mnyika na Wenzake waliomba mkopo huo kwa ajili ya kufanyia biashara zao na kwamba yeye mnyika akiwa kama Mwenyekiti wa Bodi Kampuni alitoa Dhamana ya Hadhi yake (Personal Guarantee) ya shilingi milioni 300, sambamba na mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Bwana Lazaro Obadia Mtani aliyetoa pia dhamana kama hiyo.

vielelezo vinasema hati hizo zilisainiwa na mnyika, Mtani na madirisha mbele ya mwanasheria wa kampuni hiyo Thomas Brash tarehe 11 mwezi wa Tano 2012.

baada ya kusainiwa kwa hati hizo ziliwasilishwa benki na kupatiwa mkopo huo tarehe 14.08.2012 na kuanza kurejesha rejesho la jumla ya shilingi milioni tisa na laki moja na elfu ishirini kuanzia tarehe 21.08.2012. ambapo mkopo ulipaswa kuwa wa miezi 48 mpaka mwezi Julai mwaka huu.ambapo katika kipindi chote cha awali ambacho marejesho hayakuwa yakisumbua Mnyika aliendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo ya Testa.

vielelezo zaidi vinaonyesha kwamba mpaka kufika 31.01.2014, siku ambayo TESTA ilipeleka rejesho mara ya mwisho na kushoindwa kuweza kulipa tena huku ikibakisha deni la shilingi milioni 222 na ushee, Mnyika alikuwa bado mwenyekiti wa Bodi.

taarifa za uhakika ambazo JAMVI LA HABARI linazo, zinasema miezi kadhaa mbele baada ya kampuni hiyo kushindwa kuendelea kulipa ndipo baadhi ya watu wanaomzunguka Mnyika walipomshauri Mbunge huyo ajitoe kwenye umiliki wa kampuni hiyo na kusingizia kuwa siasa zinambana huku ukweli akiujua kuwa ni kukimbia mrundikano wa madeni .

jambo linaloonekana kushangaza wengi ni kitendo cha mnyika kujitoa kimya kimya katika umiliki wa kampuni hiyo hasa baada ya kushindwa kulipa deni bila hata kuwajulisha Tumbo na Meja Chanika ambao walitoa nyumba zao kumdhamini.

akizungumza na JAMVI LA HABARI mtaalam wa masuala ya fedha Bwana Crispin Makejo amesema alichokifanya mnyika ni mchezo wa kuigiza na kwamba hana namna zaidi ya kulipa deni hilo.
'' ukikopa pesa benki, na wewe ukiwa mwenyekiti wa Bodi, na ukasaini Board Resolition, benki itakuhesabu kama wewe ndiye mkopaji na una wajibu wa kulipa deni hilo''. anasema Makejo

zaidi makejo anaongeza ''kitendo cha Mnyika kuweka Personal Guarantee, anajikanganya zaidi na kwamba Personal Guarantee inamuhitaji yeye kurejesha deni hilo katika hali yoyote ya kipato chake hata kama amefilisika''.

siku za hivi karibuni Mnyika alinukuliwa na Gazeti mola la Kiswahili (Sio JAMVI LA HABARI) Kuwa hausiki na kampuni hiyo na kwamba alishajitoa kwenye kampuni hiyo bila kusema amejitoa lini, na anataka nani amlipie deni alilokopa yeye mwenyewe.

Taarifa zilizothibitishwa na JAMVI LA HABARI zinasema kuwa Mnyika na TESTA LIMITED kwa sasa wamefilisika na hawana uwezo tena wa kulipa madeni hayo na hata meneja msimamini (Mkurugenzi mkuu) wa Kampuni hiyo bwana Obadia ameshakata tamaa ya biashara ya kampuni hiyo.

''Kinachoniumiza zaidi ni Mnyika kumtumia ndugu nyangu vibaya, kwanini hakuchukua mkopo kwa nyumba ya Mama yake ya mtoni Kichangani pale. kwanini anataka kumtia umasikini ndugu yangu?, hatuwezi kukubali hata kidogo''. anasema ndugu wa mmoja wa wadhamini.

wakati madeni ya Standard Chatered yakifikia sura hii, taarifa zinasema TESTA LIMITED ikiwa chini ya Mnyika inadaiwa zaidi ya Shilingi bilioni 1 na Benki nyingine Kadhaa.

Mpaka sasa Nyumba inayomilikiwa na Erasto Tumbo, Imeshapigwa Mnada mara mbili na kwamba jumaapili ya tarehe 02.10.2016 ilikuwa ipigwe mnada kwa mara ya tatu lakini madalali wanaohusika na suala hilo hawakufika kupiga mnada japo walitangaza.
JAMVI LA HABARI litaendelea kuwajuza juu ya kadhia hii na nyingine nyingi zinazowahusu watu wenye vipato vya kawaida na vya chini wanapoonyesha kutaka kudhulumiwa ama kupotezewa haki zao.

Chanzo: Jamvi la Habari
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top