Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Hii hapa Kauli ya mwisho ya Samwel Sitta mara baada ya kuelezwa na Daktari wa Ujerumani kuwa hatoweza kupona


Kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanza nia (2005-2010), Samuel Sitta, mwanae wa kiume ameweka wazi maneno matatu ya mwisho aliyoyatamka, yenye maana nzito katika maisha.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye ni mtoto wa kiume wa marehemu, alisema kuwa baba yake alitoa maneno matatu ya kuukubali ukweli wa maisha baada ya Daktari kumueleza kuwa asingeweza kupona.

“That’s life (hayo ndiyo maisha),”Benjamin alikariri maneno ya baba yake. Alisema hayo yalikuwa maneno yake ya mwisho baada ya kuelezwa ukweli na daktari wa hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu.

Maneo ya Sitta ni funzo kubwa kwa watu wote kuwa maisha huanza na huisha, hiyo ndiyo maana ya maisha na hakuna aishie milele hivyo tuishi kwa kuzingatia maana hiyo ya maisha na kuikubali.

Sitta ambaye anakumbukwa kwa kauli mbiu yake na matendo ya kusimamia ‘kasi na viwango’, alifariki kutokana na ugonjwa wa tezi dume uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Alitangaza kustaafu siasa muda mfupi baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ambapo yeye alikuwa mmoja kati ya waliokuwa msitari wa mbele kumnadi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo.

Benjamini alieleza kuwa marehemu atazikwa Urambo Mkoani Tabora na kwamba ratiba ya mazishi itatolewa na Ofisi ya Bunge ambayo ndiyo inayoratibu mazishi

“Tumempoteza baba na kiongozi ambaye tulikuwa tunamtegemea kwa ushauri na masuala mbalimbali, tutafuata yale aliyokuwa akituelekeza,” alisema Benjamini.

Hakika Taifa limempoteza mtu muhimu, pengo lake halitazibika kamwe. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top