Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tundu Lissu pasua kichwa


Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amemuomba radhi Hakimu Mkazi Mkuu wa Kisutu kwa kushindwa kutekeleza amri ya kumkamata mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio.

Wakili Mwita alifanya hivyo jana baada ya hakimu huyo, Thomas Simba kumuhoji sababu za kushindwa kutekeleza amri hiyo wakati hati ya kumkamata ilitolewa Novemba 3, 2016 na wakili huyo kuisaini.“Kwa nini hamkumkamata” Si mlikuwa na wajibu wa kumkamata? Mnamuogopa?”alihoji hakimu huyo.

Hata hivyo, pamoja na kuomba radhi hiyo mahakama imechukua hati ya kusafiria ya Lissu ili kudhibiti safari zake nje ya nchi kwa kuwa amekuwa akisafiri bila kuitaarifu mahakama.

Katika kesi hiyo, Lissu na watu wengine watatu wameshtakiwa kwa makosa matano ya uchocheza kutokana na habari iliyochapishwa na gazeti la Mawio kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 28, 2016 na washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.

Kabla ya uamuzi huo, Wakili Mwita alisema jana ilikuwa siku ya kesi hiyo kutajwa na kwamba upelelezi unakaribia kukamilika.

Kuhusu madai ya kudharau mahakama Wakili Peter Kibatala anayemwakilisha Lissu aliiambia mahakama kuwa mteja wake yupo mahakamani, hivyo ametii amri ya mahakama na kwamba jukumu la dhamana ni kuhakikisha mshtakiwa anakuwapo mahakamani wakati wa kesi yake na kwamba uwepo wake ni kutii masharti ya dhamana.

Hata hivyo, Wakili Mwita alidai kuwa kitendo cha Lissu kutofika mahakamani mara mbili mfululizo ni kama kuonyesha dharau kwa mahakama hiyo.

Mwita alidai kuwa Lissu ni mwanataaluma wa sheria na anafahamu taratibu za kufuatwa kama hafiki mahakamani na kwamba mdhamini si mbadala wa mshtakiwa mahakamani.

“Alipaswa kuandika barua kuitaarifu mahakama hii kama wakili kuwa ana kesi ya uchaguzi anayoiendesha Bunda na kuambatanisha na samansi ama orodha ya kesi. Tunaomba mahakama iheshimiwe na jukumu la kumfutia dhamana ama kutokumfutia dhamana Lissu bado lipo mikononi mwako mheshimiwa,” alieleza wakili huyo wa Serikali.

Akizungumzia hoja hizo, Hakimu Simba alisema Lissu ni wakili maarufu, msomi na anajua taratibu zote za mahakama, lakini wadhamini wake wanababaika, hivyo alimtaka aeleze sababu za kwenda Ujerumani bila kutoa taarifa mahakamani.

Lissu alijibu kuwa hakuwa na nia ya kuidharau mahakama, wala kuikimbia kesi inayomkabili bali alikwenda Ujerumani katika mazingira ya dharura.

Hakimu Simba alimwambia mahakama inafahamu kesi za uchaguzi na maelekezo yake, hivyo ikamuuliza sababu za kutotoa taarifa wakati alipokwenda kushughulikia kesi ya Bunda 

“Nilipopata taarifa ya kwenda kuiendesha kesi hiyo ilikuwa ni siku moja baada ya kutoka nchini Ujerumani na kwamba niliandika barua ya kuitaarifu mahakama na nilituma iletwe mahakamani kupitia wasaidizi wangu,”alisema Lissu.

Lakini Hakimu Simba alisema: “Hakuna barua iliyotufikia. Usituingize katika migogoro kutokana na nafasi yako katika jamii ya mwanasheria. Hatukuogopi labda upande wa mashtaka ndio wamekuogopa.

“Tunataka kufuata mfumo, hatutakuogopa na wala hatutakuonea. Hapa naona upande wa mashtaka wanapiga blaa blaa, tuelewane tunaichukua hati yako ya kusafiria ili ukitaka kusafiri tujue.”
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top