WADAU wa maegesho jijini Dar es Salaam, wameilalamikia mamlaka ya Jiji kwa kupandisha bei ya maegesho.
Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, wadau hao walisema mtumiaji wa huduma hiyo amekosa mtetezi kwa kuwa mamlaka zinapandisha bei hiyo bila kuwashirikisha na hawana pa kuhoji.
“Kwa sasa ukiegesha gari kwa saa moja unalipa Sh. 500, kila siku naegesha gari, sijasikia matangazo ya kutujulisha mabadiliko ya bei hizo zaidi unakuta vijana wakusanya ushuru na ukibishana nao wanaita gari la kufunga gari lako na kwenda kulihifadhi hadi ulipe faini,” alisema Mohamed Juma, mkazi wa Mbezi ambaye huegesha gari lake eneo la Posta.
Source: Nipashe
Post a Comment