Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwenyekiti mpya NEC aanza kazi rasmi kwa kishindo

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) kwenye Ofisi za Tume zilizoko Posta jijini Dar es salaam. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameapishwa leo Ikulu jijini  Dar es salaam kuiongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka 5.

  Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.

  Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) akiwa Ofisini kwake kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa leo. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake leo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top