Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli kula sikukuu ya Krismasi mkoani Singida

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 24 Desemba, 2016 amewasili mkoani Singida na kupokelewa na mkuu wa Mkoa wa huo  Dkt. Rehema Nchimbi na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Singida.

Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, leo  tarehe 25 Desemba 2016 wanatarajia kuungana na waumini wengine wa dini ya Kikristo nchini  katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi mkoani Singida.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaomba waumini wa dini ya kikristo mkoani Singida kujitokeza kwa wingi  kuungana na Rais Magufuli katika ibada ya Krismasi kwani imekuwa ni heshima kwao kutokana na uwepo wa  Rais Mkoani hapa kwa ajili ya sikukuu ya Krimass.

Dkt. Nchimbi amewataka wananchi wa mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais Magufuli na familia yake ili aendelee kuwatumikia watanzania katika kuwaletea maendeleo.

Amesema ni bahati kubwa kwa mkoa wa Singida kwa mara nyingine tena kumpokea Kiongozi huyo Mkuu wa nchi kwa kuwa katika kipindi kifupi mkoa huo pia ulimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa alipohudhuria sherehe za Maulidi.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Singida
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Singida na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akielezea ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mkoani humo ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki katika Ibada ya Siku ya Krismasi katika Kanisa mojawapo mkoani Singida.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top