Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Sheikh Ponda amtembelea Lema gerezani

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda amemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katika Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha la Kisongo. 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Noel Olevaroya, Sheikh Ponda alizungumza na Lema kwa muda usiopungua saa moja. 

“Sheikh Ponda amekutana na Mbunge wetu Lema na amekuja mahususi kumjulia hali na amemuambia hampi pole bali anampongeza kwa kukaa mahabusu muda wote licha ya kuamini anastahili kupata dhamana,” alisema Olevaroya. 

Alisema katika mazungumzo yake alimtaka Lema kuwa sauti ya wanyonge kwa kuzungumza hata kama itamfanya awe sehemu alipo hivi sasa, kwani kuna mambo mengi yanayohitaji kusemwa na hakuna wa kuyasema. 

Pia, alimsihi kutokuona kama ametengwa bali hiyo ndiyo njia ya wapigania haki na demokrasia wanayopitia, akijitolea mfano yeye binafsi.

 Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa alipotafutwa kwa njia ya simu hakupokea na alipotumiwa ujumbe mfupi hakuweza kujibu iwapo chama chake kilikuwa na taarifa ya ugeni wa Sheikh Ponda au ilikuwa ni safari binafsi. 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top