Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ambaka Mama'ke hadi kumuua

 …Kaka wa Marehemu

DAR ES SALAAM: Dunia imekwisha! Hiyo ndiyo lugha nyepesi na rahisi unayoweza kuitumia kuelezea tukio hili. Januari 11, mwaka huu Tambani, Mbande wilayani Temeke jijini hapa, kijana mdogo, Hamis Lutani Kilumbi (21) anadaiwa kumbaka mama yake mzazi, Fatuma Mohammed Matutu (48) sambamba na kumchoma visu shingoni hali iliyomfanya apate maumivu makali hadi kufariki dunia Januari 21, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 …Kaka wa mtuhumiwa

HII HAPA SIMULIZI YAKE

Akizungumza kwa uchungu na Amani wakati wa mazishi ya mwanamke huyo, mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye Mohammed Ali, alisema kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa ambaye ni mdogo wake anayemfuata kuzaliwa, alifika nyumbani kwao, alipokuwa akiishi mama yake majira ya mchana lakini hakumkuta.

“Baada ya kumkosa mama, alikuja nyumbani kwangu maana si mbali na anapoishi mama. Lakini pia mimi, mke wangu na mdogo wetu wa mwisho wa kike, Asma, ambaye naishi naye hatukuwepo. Kwa hiyo, Hamis aliacha ujumbe kuwa, tukirudi tupewe taarifa yeye alifika na mama alikuwa anatuhitaji.
 …Marehemu  Fatuma Mohammed Matutu 48 enzi uhai wake.

UJIO WA MTUHUMIWA WATIA SHAKA

“Sasa baada ya mimi kurudi nyumbani na kupewa taarifa hizo nilishangaa sana, kilichonishangaza si kuitwa na mama bali ujio wa Hamis nyumbani kwangu, maana nilikuwa sijaonana naye kwa muda usiopungua mwaka mzima kwa vile tuliwahi kutofautiana nikampiga marufuku kuja nyumbani kwangu na yeye akaahidi akiniona popote atanipiga na nondo,” alisema Mohammed.

Hata hivyo, Mohammed alisema baada ya kuuliza juu ya wito wa mama yake, aliambiwa kuwa, Asma alishakwenda nyumbani na hakuwa anawaita kama alivyosema Hamis.

Mohammed akaendelea kueleza kuwa, baada ya maelezo hayo, aliamua kuendelea na mambo yake na alikwenda kutazama mechi ya mpira wa miguu kati ya Simba na Yanga runingani zilizokuwa zikicheza Zanzibar.

MLANGO WAGONGWA, WATOLEWA UJUMBE MBAYA

“Baada ya mechi nilirudi nyumbani na kulala. Jambo ambalo sikulitegemea ni kwamba, kufika usiku wa manane, ilikuwa yapata kama saa 8 hivi, majirani wa nyumbani kwa mama walikuja kunigongea, wakaniambia mdogo wangu Hamis anamuua mama.

“Nilikimbia mpaka eneo la tukio. Kiukweli nilimkuta mama akiwa na hali mbaya, alikuwa akivuja damu sana, kitenge na kanga alizokuwa amevaa vilikuwa vimelowa damu chapachapa.”

“Niliumizwa mno na hali aliyokuwa nayo mama. Nilimuuliza nini kilimpata na kauli yake ya mwisho alisema; ‘mdogo wako Hamis anataka kuniua.’ Bila kupoteza muda, haraka tulimbeba mama na kumkimbiza kwa mwenyekiti lakini hatukumkuta, tukampeleka kwa mjumbe, akatuandikia karatasi kwa ajili ya kumkimbiza polisi.”

MAJERUHI ALALA NA MAUMIVU

Mohammed alizidi kusimulia kuwa, kutokana na mazingira wanayoishi, haikuwa rahisi kumkimbiza muda huohuo, wakasubiri kupambazuke kwanza na alfajiri walimpeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai, wakaandikiwa PF3 na kisha kumpeleka Hospitali ya Temeke.MADAKTARI WABAINI MAZITO

Mohammed: “Mama alifanyiwa vipimo na madaktari walithibitisha kuwa, aliingiliwa kinyume na maumbile lakini pia alichomwa visu shingoni. Alianza kupewa matibabu lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya, tukamhamishia Hospitali ya Muhimbili kwenye wodi ya Kibasila. Bado hali ilizidi kuwa mbaya zaidi na Jumamosi ya tarehe 21, alipoteza maisha.”

Mwili wa Marehemu ukitolewa Mochwari

                             …Jeneza likiandaliwa kuswa.liwa


…Mwili ukiswaliwa

HUYU HAPA KAKA WA MAREHEMU

Naye kaka wa marehemu, Said Matutu, mkazi wa Mbagala Kokoto, Dar  alisema kuwa, amesikitishwa sana na tukio hilo lililosababisha kifo cha dada yake na kuongeza kwamba, mtuhumiwa anatafutwa na polisi ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Kiukweli hili suala linasikitisha mno, huwezi kumfanyia mama yako mzazi kitendo kama hicho. Huo ni unyama uliopitiliza, mtu wa namna hii ni wa kuogopwa katika jamii,” alisema Said ambaye msiba ulifanyikia nyumbani kwake.TABIA ZA MTUHUMIWA

Hata hivyo, kaka huyo aliongeza kuwa, kabla ya tukio hilo alikuwa akipata malalamiko kutoka kwa dada yake (marehemu) juu ya tabia za uvutaji bangi, utovu wa nidhamu na tabia nyingine nyingi mbovu alizokuwa nazo mtuhumiwa, lakini pia aliwahi kuambiwa kijana huyo alikuwa ni mmoja wa vijana wahalifu maeneo ya Posta Mpya.MAZISHI YAKE

Marehemu Fatuma alizikwa Jumatatu iliyopita kwenye Makaburi ya Mbagala Mponda na ameacha familia ya watoto wanne, akiwemo mtuhumiwa.KAMANDA WA POLISI TEMEKE

Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, SSACP Gilles Muroto, alipotafutwa na mwandishi wetu na kuulizwa kuhusu tukio hilo, alisema taarifa hizo bado hazijamfikia lakini atafuatilia ili kujua kilichotokea.

Source: Global Publisher
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top