Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

China kujenga viwanda 200 nchini

VIWANDA takribani 200 vinatarajiwa kuwekezwa nchini na Serikali ya China kabla ya mwaka 2020.

Mpango huo unaoenda sambamba na mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2016/2020 na pia ahadi za Rais John Magufuli ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga alisema jana alipozungumzia ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China nchini, Wang Yi itakayofanyika Januari 9, mwaka huu.

Alisema Desemba 2015, kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika na China, Tanzania ilichaguliwa kuwa miongoni mwa nchi nne Barani Afrika zitakazowezeshwa kupiga hatua kwenye maendeleo ya viwanda.

Kasiga alisema kwa mpango huo, ni matarajio kuwa watanzania takribani 200,000 watanufaika na ajira kupitia mpango huo mahsusi wa kuendeleza viwanda.

Akizungumzia ziara hiyo ya Waziri huyo wa China Wang Yi, alisema mgeni huyo atapokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga.

Alisema katika ziara hiyo, Wang atakutana na Rais John Magufuli kwa lengo la kumsalimia.

Alisema Wang na Dk Mahiga watazungumzia miradi mingine ya miundombinu, ambapo China imeahidi kuisaidia Tanzania ikiwa ni pamoja na maboresho makubwa ya reli ya Tazara, ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na ujenzi wa Reli ya Kati.
Download Our App

1 comments:

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top