Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HASHIMU RUNGWE HAJIELEWI KUWA HAELEWI?Nimepata kutazama kipande cha video kinachomuonesha Hashimu Rungwe Spunda, Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) akishangaa juu ya watu wanaosema nchi inanyooshwa wakati hajui ni wapi ilipopinda!

Kwanza nimpongeze kwa kuweza kueleza mambo kadha wa kadha mazuri ambayo yamefanywa na Serikali za CCM. Lakini ndio huyu huyu Rungwe nyakati zote amekuwa akiziponda Serikali za CCM kuwa hazijafanya chochote. Tuseme ufahamu umempata wakati akitaka kuisema Serikali ya Rais Magufuli ili amsifie Kikwete aliyekuwa akimtaja mara kwa mara?

Rungwe anataka kusema nchi ilikuwa sawasawa wakati kulikithiri rushwa, ubadhirifu, nidhamu mbovu kwa watumishi wa umma, mapato ya Serikali kuishia mifukoni mwa wajanja wachache, ufisadi, uwajibikaji wa ovyo kwa  watumishi wa umma! Ni kweli Rungwe alikuwa hayaoni haya? Ama anadhihirisha hajielewi kuwa haelewi kiwango hiki?

Leo hii nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma vimerejea; Rushwa na ubadhirifu Serikalini vimepungua; Matumizi makubwa ya pesa yasiyo na tija kwa watumishi wa umma yamepungua; kulipana posho na safari za nje zisizo na tija zimepungua kama sio kuisha kabisa. Bado najiuliza Rungwe haelewi haya ama hajielewi kuwa haelewi?!

Rungwe ametudanganya tena kwa kusema wakati Kikwete anaingia madarakani kulikuwa na vyuo vikuu 3 jambo ambalo si kweli. Kikwete wakati anaingia madarakani kulikuwa na vyuo vikuu 26. Ni kweli Rungwe hajielewi kuwa haelewi au aliamua kudanganya kwa maksudi?

Katika Mwaka mmoja wa utawala wa Serikali ya Rais Magufuli tumeshuhudia nchi ikisonga mbele, tumeona mengi mazuri yakiwemo kuzibwa kwa mianya ya upotevu wa mapato na hivyo kupelekea mapato kuongezeka kutoka makusanyo ya Tsh bilioni 800 hadi kufikia Trilioni 1.5 kwa mwezi; utolewaji wa ELIMU BURE kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari; kununuliwa kwa treni na mabehewa ya treni; kununuliwa kwa ndege mbili mpya na hivyo kuanza kulipa uhai shirika letu la ndege lililokuwa limekufa kabisa.

Rungwe anasema hakukuwa na haja ya kununua ndege wakati kuna boti na meli za kisasa. Yaani mtu anayeishi Mtwara ataendaje Arusha kwa boti au meli? Mtu wa Dar ataendaje Kigoma kwa meli? Mtu wa Mbeya ataendaje Mwanza kwa Boti?

Bado najiuliza dhamira ya Rungwe ni ipi hadi kufikia hatua ya kuudanganya umma wa Watanzania?

Na Emmanuel J. Shilatu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top