Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Breaking news .... Diwani mwingine tena wa Chadema ahamia CCMNapenda Kutoa Taarifa Kwa Umma Wa Wananchi Wa Kata Ya Maroroni Kuwa Diwani Wa Chadema Na Mwenyekiti Wa Kamati Ya Ardhi Na Mazingira Ndugu Bryson Issangya Ameamua Kujiuzulu Nafasi Yake Ya Udiwani Kwenye Kata Hiyo Kuungana Na Juhudi Nzuri Za Mh. Rais John Pombe Magufuli Kwa Utendaji Wake Mzuri Wenye Dhamira Njema Kwa Taifa.


Diwani Huyu Wa Chadema Ni Diwani Wa Tatu Hapa Wilayani Arumeru Mashariki Kujiuzulu Kwenye Nafasi Hiyo Kutokana Na Kazi Kubwa Inayofanywa Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Chini Ya Mkuu Wa Wilaya Ndugu Alexander Pastori Mnyeti Kwa Uchapakazi Wake Bila Kubagua dini, kabila, Rangi Wala Chama Na Kuweka Kipaumbele Maendeleo Ya Wananchi Mbele Kwa Mantiki Hiyo Basi Ameamua Kujitoa Chadema Ili Aweze Kushirikiana Na Mh. Rais Magufuli Kuwatumikia Wananchi Wa Maroroni Na Wilaya Nzima.


Mintarafu Diwani Bryson Issangya Anasema Vita Ya Kiuchumi Pamoja Na Vita Vingine Anavyopambana Mh. Rais Magufuli Ndio Maono Yake Ya Muda Mrefu Aliyokuwa Anapambana Kuyaona Yatokee Na Sasa Ni Shuhuda Wa Macho Ya Nyama Hivyo Dhamira Yake Inamsuta Kumpinga Rais Magufuli Wakati Anatenda Kwa Matendo Ahadi Zote Alichosema.


Mathalani Diwani Bryson Issangya Amekiri Wazi Kwamba Kwenye Kamati Aliyokuwa Anasimamia Kwenye Halmashauri Ya Arumeru Ya Ardhi Na Mazingira Ilikuwa Na changamoto Nyingi Kutokana Na Baadhi Ya Madiwani Wenzake Wa Chadema Kuwa Na Migogoro Isiyokwisha Kila Wanapopanga Inamwia Vigumu Kutekeleza Kwa Weledi Kutokana Na Maslahi Binafsi Ya Madiwani Hao Hivyo akaona Akae Pembeni Na Kuungana Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Ya Rais Magufuli Ambayo Inafanya Kazi
Na Kuweka Siasa Pembeni Na Kuwaomba Wananchi Wa Kata Ya Maroroni Kuungana Na DC Mnyeti Kuleta Maendeleo Yao Kwani Ana Imani Naye Kutokana Na Uchapakazi Wake.


Diwani Bryson Issangya Amekabidhi Barua Zake Zote Kwa Maandishi Kwa Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Meru  Na Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya Kama Kumbukumbu Sahihi Ya Kujiuzulu Kwake Leo Tarehe 22.06.2017.


Napenda Kutoa Pongezi Zangu Za Dhati Sana Kwa Rais John Pombe Magufuli Kwa Kazi Nzuri Anayofanya Na Kupata Uungwaji Mkono Toka Viongozi Wa Asasi Mbalimbali Na Viongozi Vyama Vya Siasa Kwa Kuona Dhamira Yake Njema Kwa Taifa Hili.


Titho Cholobi.
Download Our App

1 comments:

Njaaa ya kuteuliwa tu hio dogo kapata bei

Reply

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top