Viongozi wawili wa serikali za mtaa katika Kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti mkoani Pwani wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumatano, Juni 28.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga zimeeleza kuwa waliouawa ni Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi, Shamte Makawa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.
Aidha, kamanda wa polisi amesema kuwa tayari askari wamekwenda eneo hilo kwa ajili ya hatua zaidi.
Hadi sasa watu zaidi ya 37 tayari wameuawa katika mfululizo wa matukio ambayo bado Polisi hawajafahamu ni nani mhusika na lengo haswa la kufanya hivyo
Post a Comment