Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAJAMBAZI WANNE WAUWAWA NA POLISI KIBITI
Jeshi la Polisi Tanzania mnamo tarehe 29/06/2017 saa tatu kamili usiku huko katika kijiji cha PAGAE wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, kwenye barabara inayotoka Pagae kuelekea Nyambunda.

Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita wakitokea barabara kuu ya lami wakifuata barabara hiyo inayoelekea Nyambunda kilomita 100 kutoka barabara kuu.

Watu hao walipogundua kuwa watu waliokuwa mbele yao ni Askari Polisi walikimbia vichakani na ghafla wakaanza kuwashambulia askari kwa risasi.

Askari Polisi walijibu mapigo na kuanza kupambana na watu hao.

Katika mapambano hayo askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wanne katika kundi hilo la wahalifu hao.

Aidha katika mapambano hayo zilipatikana silaha mbili aina ya Smg na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao.

Watu hao wanne ambao wanasadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaendesha vitendo vya mauaji katika wilaya za Mkoa wa Pwani.

Majeruhi hao walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa hospitali kutokana na kuvuja damu nyingi zilizotokana na majeraha ya risasi waliyopata, milli ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi zitakazosaidia kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivi vya kihalifu kwenye wilaya za Mkoa wa Pwani.

Imetolewa na;
L.SABAS -DCP
MKUU WA OPARESHENI MAALUM ZA JESHI LA POLISI TANZANIA.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top