Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Vigogo Escrow, IPTL wapandishwa kizimbani .... Video kamili ipo wakipandishwa mahakamani

TAKUKURU inawashikilia Singh Sethi na Rugemalila(Waliotajwa kashifa ya Escrow ) kwa tuhuma za uhujumu uchumi

- Kupelekwa Mahakamani

TAKUKURU imesema inawafikisha mahakamani watuhumiwa, James Rugemarila na Harbinder Sethi kwa makosa ya uhujumu uchumi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewafikisha mahakamani, mmiliki kampuni ya PAP, Habirnder Seth Singh na mfanyabiashara James Rugemalira kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumatatu, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola amesema, “Leo nawapa taarifa kuwa tunawafikisha mahakamani watuhumiwa wawili, kwa makosa ya kuhujumu uchumi na mengine yanayofanana na hayo.”
Amesema kwa muda mrefu amekuwa akiulizwa kesi za Escrow na kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) zimeishia wapi, hivyo taasisi hiyo imechunguza shauri hilo kwa muda mrefu na kujiridhisha kwamba linaweza kufikishwa mahakamani.

“Kwa hatua ya awali wataenda Mahakama ya Kisutu, baada ya hapo kuna utaratibu wa kimahakama, watapelekwa mahakama maalumu kutokana na kiwango cha hujuma kilichofanyika na fedha zilizohusika,” amesema Mlowola.

TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top