Miongoni mwa mastaa aliowataja ni pamoja na Wastara, Johari na wengine ambapo kutokana na maelezo yake hayo, gazeti hili liliona ni vyema kupata uthibitisho wa kile alichokisema kabla ya kuandika gazetini.
PATRICK ATOA USHAHIDI
Baada ya kubanwa sana ikiwa ni pamoja na kuambiwa kuwa anatafuta kiki kwa kudai alitoka na mastaa hao wakati hana jeuri hiyo, Patrick alimfowadia paparazi wetu ‘chatting’ aliyokuwa anafanya na Wastara kupitia Mtandao wa WhatsApp wakati walipokuwa wapenzi.
Kwenye ‘chatting’ hiyo zilionekana baadhi ya meseji ambazo zilikuwa chafu hali iliyomfanya mwandishi azitilie mashaka kama kweli zilitoka kwa Wastara kwenda kwa mwanaume huyo ama kuna kitu kinaendelea.
Baada ya kupata madai hayo ya Patrick na ‘chatting’ ambayo ‘ameikapcha’ kwenye simu yake iliyokuwa sambamba na picha na video romantic za Wastara, alizodai kuwa alikuwa akimtumia jamaa huyo, mwandishi wetu aliona ni busara kumtafuta Wastara ili aifungukie skendo hiyo nzito iliyomganda.
Alipopatikana kupitia simu yake ya mkononi alifunguka hivi: “Huyo mtu simjui na picha nimeziona wamezitengenezatengeneza tu kwa maana hakuna picha yoyote ambayo labda kusema nimekaa naye nipo utupu ama kuna kitu nafanya naye. Huyo mtu anatafuta kiki kwani ameshamchokonoa kila mtu na wote wamemkimbia.
“Sina mazoea naye yoyote zaidi ya siku moja kunitafuta na kuniambia anataka kutengeneza video ya muziki akaja kuniletea vitu vingine tokea hapo nikamjibu mbaya. Kama kuna video ipo nimemtaja jina lake sawa ila ninachojua hakuna kitu kama hicho.
“Nilishamtukana asinizoee! Sijaishi katika mazingira hayo, sijapata ustaa kwa kuchati na wanaume, iweje mtu aje kuniharibia jina langu nililotengeneza kwa miaka mingi. Sijapendwa na watu kwa kukaa utupu.”
Post a Comment