Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

YALIYOJIRI ZIARA YA MHE. RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI - KIBAHA, MKOANI PWANI - JUNI 20, 2017.


#"Mkoa wa  Pwani una jumla ya viwanda 371" - Eng. Ndikilo.

#"Agenda ya ujenzi wa viwanda inazungumzwa kwa lugha moja kwa viongozi wa Serikali ya mkoa na Chama Cha Mapinduzi," - Eng. Ndikilo.

#"Ifikapo Desemba 2017, Pwani  itakuwa na viwanda vingine vikubwa 10," - Eng. Ndikilo.

#"Nina wajibu mkubwa wa kuwatumikia Watanzania bila kujali vyama vyao," - Rais Dkt. Magufuli.

#"Ahadi nilizozitoa wakati wa kampeni, namuomba Mungu anisaidie niweze kuzitimiza," - Rais Dkt. Magufuli.

#"Tanzania ni ya pili baada ya Brazil kwa kuwa na vivutio vingi Duniani," - Rais Dkt. Magufuli.

#"Elimu bure imeongeza uandikishaji wa wanafunzi kutoka wanafunzi Mil 1 mwaka 2015 kufikia Mil 2 mwaka 2016," -  Rais Dkt. Magufuli.

# "Tumenunua ndege mpya 6 kwa kutumia fedha  tunazozikusanya," - Rais Dkt. Magufuli.

# "Tumeanza kujenga Reli ya kimataifa kwa fedha tunazozikusanya ndani ya nchi," - Rais Dkt. Magufuli.

# "Mkoa wa Pwani, unaongoza kwa kuwa na viwanda vingi nchini," - Rais Dkt. Magufuli.

# "Mkoa wa Pwani hauna madini ya chuma lakini una kiwanda cha chuma, lakini kuna mikoa yenye madini ya chuma na haina hata viwanda vya misumari" - Rais Dkt. Magufuli.

#"Viwanda hivi vyote vitatengeneza ajira kwa watoto wetu badala ya kushindia viroba," - Rais Dkt. Magufuli.

#"Lengo langu ni kutengeneza ajira kwa watoto wa Kitanzania," - Rais Dkt. Magufuli.

# "Ninawaomba wana Kibaha na Pwani tushikamane katika ujenzi wa viwanda," - Rais Dkt. Magufuli.

# "Rufiji hakuna kiwanda sababu tumejichelewesha wenyewe," - Rais Dkt. Magufuli.

#"Tumeongeza fedha zinazopelekwa katika miradi ya maendeleo kutoka 20% mpaka 40%," - Rais Dkt. Magufuli.

#"Nataka kila kiongozi katika nafasi yake ajitathimini anavyowajibika kwa wananchi wa hali ya chini," - Rais Dkt. Magufuli.

#"Wananchi wanamatumaini makubwa na Serikali ya awamu ya Tano," - Rais Dkt. Magufuli.

# "Uongozi wa Mkoa wa Pwani umenifurahisha kwa kuanzisha ujenzi wa viwanda," - Rais Dkt. Magufuli.

# "Niliamua kwa makusudi Wizara ya TAMISEMI iwe chini yangu, ili niweze kusimamia mimi mwenyewe," - Rais Dkt. Magufuli.

# "Hadi kufika 2020, vijiji vyote vya mkoa wa Pwani vitakuwa vimepata umeme," - Rais Dkt. Magufuli.

# " Ninawashukuru wananchi wa Kibaha na Mkoa wa Pwani kwa mapokezi mzuri", - Rais Dkt. Magufuli.

# " Wana-Kibaha na Wana-Pwani mkawe waaminifu katika viwanda vinavyoanzishwa," - Rais Dkt. Magufuli.

Imeandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO).
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top